Jumatano 3 Juni 2026 - 11:10
Pakistan yatangaza kuendelea kuiunga mkono Palestina licha ya shinikizo la Israel

Hawza/ Pakistan, kwa lengo la kuzuia kuwepo kwa utata kuhusu msimamo wake kuhusiana na Israel, ilisisitiza kwamba; msimamo wake wa kuliunga mkono taifa huru la Palestina bado unaendelea kuwa thabiti.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Islamabad ilikanusha kwa uthabiti uvumi kuhusu kujiunga na Makubaliano ya Ibrahim ambayo yanahusishwa na utawala wa Kizayuni, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuzitaka nchi za Kiislamu kuhalalisha na kurekebisha uhusiano wao na Israel, na akalielezea jambo hilo kuwa ni sehemu ya kile alichokiona kuwa ni mpango mpana wa amani ya kikanda.

Afisa mmoja mwandamizi wa Pakistan alisema: “Ningependa kutangaza kwa uwazi kwamba; sera ya kudumu ya Islamabad ni kwamba Pakistan, mpaka Palestina itakapokuwa imetambuliwa rasmi na mpaka Palestina itakapoanzishwa kwa mujibu wa mipaka ya kabla ya mwaka 1967 ikiwa na mji wa Quds kuwa mji wake mkuu, itaendelea kuwa muungaji mkono wa taifa huru la Palestina.”

Makubaliano yanayojulikana kama Makubaliano ya Ibrahim, ambayo yamefafanuliwa na utawala bandia wa Israel, yanajumuisha makubaliano ambayo kwa uungwaji mkono wa Marekani huzifanya nchi mbalimbali kurekebisha na kuhalalisha uhusiano wao na utawala wa Israel.

Kauli za Trump zimeibua radi amali kali nchini Pakistan, kiasi kwamba vyama vikuu vya kisiasa, mashirika ya kidini, pamoja na makundi na muungano ya kiraia vimeishutumu Washington kwa kuzishinikiza nchi za Kiislamu kuitambua Israel bila kuzingatia haki za Wapalestina.

Chanzo: SHIITE NEWS

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha